Polisi sita wajeruhiwa kwenye vurugu katika mji wa The Hague
18 Februari 2024Matangazo
Vurugu hizo kati ya wafuasi na wapinzani wa serikali ya Eritrea zimesababisha pia uharibifu mkubwa wa mali. Polisi imesema maafisa wake na wahudumu wa huduma ya dharura walipigwa mawe na fataki wakati makundi hayo mawili yanayopingana yalipopambana huku ikisema watu 13 wametiwa mbaroni kufuatia mkasa huo. Magari mawili ya polisi na basi moja yameteketea kabisa, huku magari mengine yakiharibiwa vibaya. Eneo la mkutano lililoandaliwa na kundi linaloiunga mkono serikaya Eritrea pia limeharibiwa. Polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi ili kutuliza ghasia. Meyawa mji wa The Hague, Jan van Zanen, amelaani ghasia hizo na ameamrisha hali ya hatari katika eneo la tukio.