Putin akutana na viongozi wa Afrika
27 Julai 2023Katika barua yake ya kuwakaribisha washiriki, Putin amesema kuwa ushirikiano wa biashara, uwekezaji, nishati, kupunguza umasikini, kuhakikisha usalama wa chakula na mabadiliko ya tabianchi, vitajadiliwa katika mkutano huo wa kilele.
Putin pia anapanga kukutana na viongozi wa Afrika na kuendeleza mazungumzo kuhusu juhudi za mpango wa amani zinazofanywa na Afrika kwa ajili ya Ukraine.
Soma zaidi: Afrika Kusini yasifia ujumbe wa amani Ukraine baada ya mazungumzo
Ujumbe wa Afrika wakutana na Putin kuhusu mzozo wa Ukraine
Imeripotiwa kuwa wawakilishi kutoka nchi 49 kati ya 54 za Afrika watahudhuria mkutano huo unaofanyika St. Petersburg, ambapo 17 ni wakuu wa nchi na serikali.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, anaizuru Liberia, ikiwa ni ziara yake ya tatu barani Afrika tangu Urusi ilipoivamia nchi yake mnamo Februari 2022.