SiasaUkraine
Putin anusurika na uasi wa kundi la Wagner
25 Juni 2023Matangazo
Hii ni baada ya Rais Vladimir Putin kuafikiana na makubaliano ya msamaha ili kusitisha uasi.
Makubaliano hayo yanaonekana kusitisha kitisho kuwa kundi hilo, chini ya kiongozi wao Yevgeny Prigozhin linaweza kuivamia Moscow.
Soma pia: Rais wa Urusi Vladimir Putin asema uasi wa mamluki wa Wagner ni usaliti.
Mzozo wa muda mrefu kati ya Prighozin na viongozi wa kijeshi juu ya uendeshaji wa operesheni ya Urusi huko Ukraine ulizidi siku ya Jumamosi, vikosi vya Wagner vilipochukua udhibiti wa kambi muhimu ya jeshi la Urusi katika mji wa Rostov-on-Don.
Putin alishutumu hatua hiyo kama uhaini na kuapa kuwaadhibu wahalifu, akiwatuhumu kwa kuisukuma Urusi kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.