Raia wa Gabon wapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya
17 Novemba 2024Serikali ya Gabon inasema kura hiyo inatoa fursa kwa nchi hiyo kurejea kwenye utawala wa kidemokrasia na kufungua ukurasa mpya baada ya miaka 55 ya utawala wa kifamilia katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta barani Afrika.
Soma Pia: Viongozi wa kijeshi wa Gabon watangaza kuandaa uchaguzi 2025
Katiba mpya inaweka ukomo wa mihula miwili ya urais. Muhula mmoja wa urais utakuwa wa miaka saba. Katiba inayopendekezwa pia itaondoa nafasi ya waziri mkuu na kutambua Kifaransa kama lugha rasmi itakayotumika katika shughuli za Gabon. Rais wa mpito, Brice Oligui Nguema, aliwataka wapiga kura kuidhinisha hatua hizo, ambazo amesema zitasaidia Gabon kupanga mkondo mpya wa taifa hilo.
Takriban watu milioni 1 walitarajiwa kupiga kura. Matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutolewa muda wowote kuanzia sasa na mahakama ya kikatiba itatangaza matokeo rasmi, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Gabon.