Raia wa Iran wanapiga kura leo kumchagua rais mpya
28 Juni 2024Matangazo
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi saa za Iran na vinatarajiwa kufungwa saa kumi na mbili jioni japo zoezi hilo linaweza kuendelea hadi saa sita za usiku.
Uchaguzi huo ulioandaliwa kwa haraka unatokea katikakati ya mvutano wa kikanda juu ya mzozo kati ya Israel na Hamas, pamoja na ongezeko la shinikizo kutoka mataifa ya Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Soma pia: Wairan waelekea vituoni kumchagua rais mpya kumrithi Raisi
Wachambuzi wameeleza kuwa, matokeo ya uchaguzi wa leo hayawezi kuleta mabadiliko makubwa katika sera za Jamhuri hiyo ya Kiislamu lakini yanaweza kuamua ni nani atakayemrithi kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei, aliyekuwa madarakani tangu mwaka 1989.