Rais Jammeh akabiliwa na upinzani mkali kwenye uchaguzi
30 Novemba 2016Matangazo
Rais Jammeh anayelaumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika uongozi wake wa miaka 22, aligonga vichwa vya taarifa za vyombo vya habari duniani pale alipotangaza kuiondoa nchi yake kutoka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwezi Novemba.
Kiongozi huyo aliwahi pia kuitangaza kuwa nchi yake kuwa Jauhuri ya Kiisalamu na katika tukio jingine alisema ametengeneza dawa ya kutibu ugonjwa wa UKIMWI kwa kutumia kitabu kitakatifu cha Qur'an.
Rais Yahya Jammeh alitwaa madaraka mwaka 1994 baada ya kumpindua Rais Dawda Jawara.