Rais Ouattara wa Ivory kuwania tena Urais Oktoba
7 Agosti 2020Matangazo
Rais Ouattara amesema ameitikia wito wa wananchi waliotaka awanie Urais.
Kinyangan'yiro cha Urais kilichukua mwelekeo mwengine baada ya waziri mkuu Amadou Coulibaly aliyeonekana kuwa chaguo la Ouattara kama mrithi wake kufariki kwa ugonjwa wa moyo mnamo Julai, 8 akiwa na umri wa miaka 61.
Hata hivyo, uamuzi wake wa kujitosa kwenye kinyangan'yiro cha Urais huenda ukaibua tuhuma za ukandamizaji wa demokrasia wakati wa mihula yake miwili uongozini.
Hapo awali, aliwahi kusisitiza kufanyike mabadiliko ya katiba ili kumuwezesha kuwania muhula wa tatu madarakani.
Miongoni mwa wagombea wengine ni pamoja na aliyewahi kuwa waziri mkuu katika utawala wa Gbagbo Pascal Affis, Henri Konan, na waziri wa zamani wa mambo ya nje Marcel Amon Tanoh.