Rais Volodymyr Zelensky ataka Urusi kushinikizwa zaidi
19 Novemba 2024Zelensky ametowa mwito huo katika hotuba yake aliyoitowa kwa njia ya video, mbele ya bunge la Ulaya kuhusu maadhimisho ya siku 1,000 tangu Urusi ilipoivamia nchi yake.''Kwa pamoja tumefanikisha mengi. Lakini hatupaswi kukhofia kuchukua hatua zaidi. Putin amewaleta wanajeshi 11,000 kutoka Korea Kaskazini na kuwapeleka katika maeneo ya mipaka ya Ukraine. Kikosi hiki huenda kikaongezeka hadi wanajeshi laki moja wakati baadhi ya viongozi wa Ulaya wakiwa bado wanatafakari kuhusu hilo,na wengine wakiwaza juu ya uchaguzi au mambo kama hayo, huku wakiitowa muhanga Ukraine,na Putin akilenga kushinda vita hivi. Hawezi kusitisha vita hivi kwa hiyari.'' Rais wa bunge la ulayaRobertaMetsola amesema Umoja huo utaendelea kusimama na Ukraine huku mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Mark Rutte, ambaye amezungumza katika kikao cha mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya, akionya kwamba rais Vladmir Putin hapaswi kuachiwa kushinda nchini Ukraine.