SiasaIran
Rais wa Iran kufanya ziara nchini China
12 Februari 2023Matangazo
Hayo yamefahamishwa leo na vyombo vya habari vya serikali ya Tehran na kusema kuwa Rais atajibu mwaliko wa Rais wa China Xi Jinping.
Marais hao wawili walikutana kwa mara ya kwanza Septemba mwaka jana nchini Uzbekistan katika mkutano wa kilele wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai, ambapo rais wa Iran alitoa wito wa kuimarisha uhusiano.
Fahamu zaidi:
Iran na China zina uhusiano mkubwa wa kiuchumi, hasa katika nyanja za nishati, usafiri, kilimo, biashara na uwekezaji. Nchi zote mbili zilitia saini mwaka 2021 "mkataba wa ushirikiano wa kimkakati" wa miaka 25 unaosemekana kujumuisha vipengele vya "kisiasa, kimkakati na kiuchumi".