Rais wa Tanzania azungumzia kuporomoka kwa ghorofa
18 Novemba 2024Matangazo
Rais Samia amesema hadi sasa hawajafahamu sababu za kuanguka kwa jengo hilo, huku akiyashukuru mashirika, wadau na wataalamu wa afya kwa msaada wao.
Aidha rais Samia amesema serikali itagharamia matibabu na kusaidia katika taratibu za mazishi. Kuporomoka kwa majengo hutokea katika baadhi ya miji ya Afrika kutokana na udhaifu wa viwango vya ujenzi na wakati mwingine uzembe wa utekelezaji wa sheria.
Watu 13 wamethibitishwa kufariki na wengine zaidi ya 80 wamejeruhiwa nchini Tanzania, baada ya jengo la ghorofa kuporomoka Jumamosi iliyopita katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.