Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo, yuko huru kusafiri
7 Septemba 2023Matangazo
Katika taarifa yake iliyotolewa kupitia televisheni ya taifa, Rais wa mpito Jenerali Brice Oligui Nguemaamesema Bongo ana uhuru wa kutembea na anaweza hata kusafiri kwenda nje ya nchi kupata matibabu kutokana na hali ya afya yake.
Soma pia: Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo aachiwa huru
Rais huyo aliyepinduliwa, alipata maradhi ya kiharusi Oktoba 2018 yaliyomsababishia ulemavu wa mwili hasa katika kusogeza mguu na mkono wa kulia.
Soma pia: Jumuiya ya ECCAS yaisimamisha uanachama Gabon
Bongo aliyekuwa madarakani kwa miaka 14, amekuwa akishikiliwa nyumbani kwake tangu jeshi la nchi hiyo lilipoipindua serikali yake Agosti 30 muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliotajwa na wanamapinduzi hao kuwa wa udanganyifu.